Genesis 36:20-25

20Hawa ndio walikuwa wana wa Seiri, Mhori, waliokuwa wakiishi katika nchi ile: Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana,
21Dishoni, Eseri na Dishani. Hawa ndio wana wa Seiri huko Edomu waliokuwa wakuu kwa Wahori.

22 Wana wa Lotani walikuwa:
Hori na Homamu. Timna alikuwa dada yake Lotani.

23 Wana wa Shobali walikuwa:
Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu.

24 Wana wa Sibeoni walikuwa:
Aiya na Ana. Huyu Ana ndiye aligundua chemchemi ya maji moto jangwani alipokuwa akichunga punda za Sibeoni baba yake.

25 Watoto wa Ana walikuwa:
Dishoni na Oholibama binti wa Ana.
Copyright information for SwhKC